Chuo Kikuu cha Mzumbe kimetia saini yamikataba mitano yenye thamani ya sh Bil 16.5 kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa miundombinu ya majengo ya chuo hicho katika kampasi ya Tanga.
Mikataba hiyo yenye thamani ya Billioni 16.5 imesainiwa leo Agosti 30.2024 Katika Kata ya Gombero Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga huku zoezi hilo likisimamiwa na Naibu Waziri wa maliasili na utalii Dustan Kitandula ili kuanza rasmi utekelezaji wa miundombinu ya majengo katika chuo hicho.
Miradi itakayotekelezwa katika Kampasi ya Tanga ni pamoja na Ujenzi wa jengo la Taaluma yenye ofisi 35 za watumishi 65, maktaba ndogo ya wanafunzi 80 na ukumbi wa mihadhara mmoja kwa wanafunzi 300
Pia Ujenzi wa Hosteli mbili za wanafunzi, Cafeteria moja yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 180, jengo la zahanati, nyumba nne za watumishi pamoja na ujenzi wa mfumo wa kusafishia maji chafu.
Mradi huo ulianza rasmi tarehe 13.09.2021 baada ya mkataba kati ya Benki ya Dunia na Serikali ya Tanzania kusainiwa Kupitia Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kiuchumi (heet project)unaofadhiliwa na Benki ya dunia ambao umelenga kuongea udahili sambamba na ubora wa Elimu, mradi huo unatakiwa kutekelezwa kwa miaka mitano.