Mix

Umeisikia ya waumini kusali wakiwa hawana nguo?? Kilichofuatia je?

on

Praying-hands-with-bible

Malalamiko yalikuwa mengi tangu kufunguliwa kwa kanisa hilo la Healing Ministry katika Kaunti ya  Machakos, Kenya.. wanawake wanaingia kwenye migogoro na wanaume zao kisa ibada, wakatu mwingine walikua wanaenda kulala hukohuko.

Hii kitu ikaleta migogoro mingi kwenye baadhi ya familia, baadae kukawa na malalamiko kwamba wanawake wanaosali kwenye Kanisa hilo wanasali wakiwa wamevua nguo zote.. siku moja watu wa eneo hilo wakavamia kanisani hapo usiku, wakakuta wanawake wakiwa wanasaliwa huku wamevua nguo zote.. Kasisi akajitetea kwamba alikuwa akiwafanyia ibada maalum.

Mwenyekiti wa muungano wa wafanyabiashara eneo hilo Duncan Mutua amesema; “Tulivamia kanisa hilo na kumfumania Kasisi akiwamwagilia wanawake maji wakiwa uchi wa mnyama alijitetea akisema alikuwa akiwafanyia maombi spesheli,”.

Amesema wasiwasi kuhusu shughuli za Kanisa hilo uliongezeka baada ya wanawake wa eneo hilo kutumia muda wao mwingi Kanisani na hata kuwaacha waume wao usiku na kwenda kwenye ibada za mkesha.

TFCHURCH2404

Hilo ndiyo kanisa ambalo limetuhumiwa kufanya ibada za wanawake wakiwa hawana nguo.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribeYouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments