Baada ya kuiongoza Azam FC katika michezo minne kwa mafanikio ndani ya mwezi November, shirikisho la soka Tanzania TFF imempa tuzo ya mwezi kocha wa Azam FC Aristica Cioaba.
Cioba ndani mwezi Novemba ameiongoza Azam FC kuvuna jumla ya point 10, wakishinda game 3 na kutoka sare mchezo mmoja.
Kwa upande wa mchezaji bora wa mwezi tuzo imeenda jijini Mwanza katika club ya Mbao FC kwa mshambuliaji wao Waziri Junior aliyefunga magoli manne katika mechi sita mwezi November.