Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, @josephkusaga amemtangaza Spencer Minja (@spencer_minja) kama Mkurugenzi Mtendaji wa Igichu Media Group ambapo pia Bodi ya Wakurugenzi imetangaza kumpa baadhi ya shares za kampuni na kumfanya moja ya wamiliki.
Igichu ambalo ni neno linalomaanisha mawingu/clouds yenye makao makuu Bujumbura, Burundi , Inamiliki radio dada ya Clouds ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuzifungua fursa nchini Burundi ikiendeleza maono ya Big Joe kuzidi kufungua dunia kwa Watanzania ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Spencer Minja ni kijana mzoefu wa masuala Uongozi na Mikakati aliyehitimu Degree ya Psychology, kabla ya uteuzi huu, amefanya kazi kama:-
1. Mtendaji Msaidizi wa Mkurugenzi wa Clouds Media Group (2024-2025).
2. Rais wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (2022-2023).
3. Mjumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
4. Mjumbe wa Bodi mbili za Unesco, National Steering Committee & Technical Steering Committee O3+.
5. Mjumbe wa Kamati ya Wizara ya Afya (GBV Frameworks & Policies).
Spencer amepokea tuzo na vyeti kadhaa vya pongezi ikiwemo, Cheti cha kutambuliwa kwa utendaji wake kwenye Bodi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mhe. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.