Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tangu tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kuvamia Clouds Media akiwa na askari wenye silaha ambapo ilifuatiwa na Waziri mwenye dhamana ya Habari, Nape Nnauye kutembelea Clouds na kuunda Kamati ambayo ingechunguza ishu hiyo. Sasa leo March 22 2017 Kamati hiyo imetoa matokeo ya uchunguzi huo.
'Kamati ilipewa kazi ya kukusanya taarifa kwa Clouds Media na RC Makonda na kutoa mapendekezo hatua ambazo zitachukuliwa'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Baadaye tulienda ofisini kwake, kamati ilipopanda ngazi mkuu wa mkoa alitokea mlango mwingine na kuondoka'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Baadaye tulienda ofisini kwake, kamati ilipopanda ngazi mkuu wa mkoa alitokea mlango mwingine na kuondoka'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'RC Makonda alichagua mwenyewe kutosikilizwa na kamati kwa hiyo haitaathiri matokeo ya uchunguzi huu'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Imebainika ni kweli alikwenda pale Clouds na askari, waliingia kwenye vyumba ambavyo walipaswa kuingia kwa idhini maalumu'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Makonda aliwatishia wafanyakazi Clouds kuwa angewafunga miezi 6 pia angewaingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Kutokana na vitisho hivyo hata kipindi cha SHILAWADU hakikufungwa kwa utaratibu wa kawaida'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Licha ya kukiri vitisho, kamati haikuona vithibitisho vyovyote kuwa walipigwa na vitako vya bunduki na kukatwa mitama'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Kamati imekuja na mapendekezo kuwa RC Makonda awaombe radhi Clouds na tasnia nzima ya habari'-Balile
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Nimeipokea ripoti, kazi hii si ndogo ina gharama kubwa'-Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Ripoti ina vielelezo vya sauti na picha za waliokuwa wanatoa ushahidi'-Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
'Sisi tuliopewa dhamana ni vizuri kujifunza kuwa wanyenyekevu, kama binadamu tunaweza kukosea lakini tunaweza kurekebisha'-Waziri Nape
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
LIVE: Waziri wa Habari Nape Nnauye anaongea na waandishi wa habari https://t.co/4RTRHgTj11
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
VIDEO: ‘Hatutaandika wala kutangaza habari za RC Makonda’ – Jukwaa la Wahariri, Bonyeza play hapa chini kutazama