Michezo

DoneDEAL: Arsenal imemsajili Pepe kwa rekodi ya club ya dau la usajili

on

Club ya Arsenal ya England imefanikiwa kukamilisha usajili wa winga wa Ivory Coast aliyekuwa anakipiga Lille ya Ufaransa Nikolaos Pepe.

Arsenal imemsajili pepe kwa mkataba wa miaka miaka mitano kwa dau la pound milioni 70 ila Arsenal watalipa kiasi hicho kwa awamu wakati Pepe akiendelea kuitumikia Arsenal.

Pepe mwenye umri wa miaka 24 msimu uliopita Ligi Kuu Ufaransa alifunga jumla ya magoli 22  na kutoa assist 11, kwa sasa Pepe ndio anakuwa mchezaji ghali zaidi ndani ya Arsenal baada ya Pierre Aubameyang aliyesajiliwa Arsenal akitokea Dortmund kwa dau la pound milioni 56 January 2018.

Soma na hizi

Tupia Comments