Baada ya chama cha soka England FA kugoma kubadilisha ratiba ya mchezo wa robo fainali ua michuano ya Carabao Cup kati ya Aston Villa na Liverpool kwa madai ya Liverpool kuwa na ratiba ngumu, leo wamekutana na changamoto hiyo.
Liverpool awali waliomba mchezo huo ubadilishwe kwa sababu wanashiriki michuano ya FIFA Club World Cup 2019 kwani wanatakiwa kucheza mchezo wao wa kwanza December 18 2019 dhidi ya Monterray nchini Qatar yaani ni ndani ya saa 24 baada mchezo dhidi ya Aston Villa.
Huku ratiba yao pia ikiwataka wacheze December 17 2019 robo fainali ya Carabao Cup, ndipo Liverpool alipoamua kupeleka kikosi A Qatar na kuacha wachezaji wa timu za viana sasa kucheza mchezo huo na kujikuta wakipigwa 5-0 na kuondolewa katika michuano hiyo.