Utafiti ulifanywa na taasisi ya GEOPOLL inayofanya kazi kwenye nchi zaidi ya 8 za Afrika umeonesha kuwa vituo vya Clouds FM na Clouds TV chini ya Clouds Media Group (CMG) vimetajwa kuwa namba moja kwenye kusikilizwa na kutazamwa zaidi Tanzania.
Utafiti huu uliofanywa kwenye robo ya mwisho ya mwaka 2016 umeonesha kuwa Clouds FM ni radio inayosikilizwa zaidi Tanzania kwa asilimia 23.6 sawa na wastani wa 7.80 ya vipindi vyake vyote wakati huo Clouds TV ikiongoza kwa asilimia 19.6.
Hapa nimekuwekea chart inayoonesha viwango vya usikilizwaji kwenye radio 10 zilizofanyiwa utafiti Tanzania.
CloudsFM imeonyesha kusikilizwa zaidi kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 4 usiku na asilimia kubwa zaidi zilizobaki kwenye asilimia nyingine zimebakia kwenye Radio za mikoani ambazo ndio zinagawana.
Television
Upande wa TV kituo cha CloudsTV kimeongoza kutazamwa kwa asilimia 19.6 ikionesha kutazamwa zaidi kaunzia saa 1 usiku mpaka saa 2 kamili usiku ambapo ITV wameongoza katika muda wa saa 2 mpaka saa 2:59 usiku.
VIDEO: Ilikupita hii ya Rais Magufuli kumtunza Mrisho Mrisho Mpoto? Nimekuwekea hapa chini.