Duniani

Wachina hawana utani, kesi ya kuwinda ndege tu unakutana na kifungo miaka 10 jela ..!!

on

Unajua ukizitaja nchi ambazo zimekuwa zikizungumziwa sana kuwa na sheria ngumu na kali, China nayo imo… unaweza kuona ishu ya kukamatwa unawinda ndege ni kesi ndogo lakini sio kesi ndogo kwa Wachina.

Vijana wawili ambao ni wanafunzi wa Chuo wamejikuta kwenye mikono ya Mahakama na kesi ya kujibu kwa tuhuma za kuwinda ndege ambao wamo kwenye list ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka.

Kesi yao ilikuwa kwenye Mahakama ya Huixian county na hukumu kutoka Mahakamani hapo inasomeka hivi; kila mmoja wao amepigwa faini ambayo ni sawa na Tshs. Mil.3.2 kwa kosa la kuwinda ndege hao na pia kuwauza, na mwisho wa yote ni kifungo cha miaka 10 na miezi sita kila mmoja jela.

Jamaa walinaswa baada ya kuwinda ndege hao 12, mmoja alikufa mwingine akatoroka.. wengine 10 waliwauza kwa njia ya mtandao  ambapo jumla ya pesa waliyopata inagusa kama laki tatu na nusu tu !!..

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments