Duniani

Camera zilivyonasa tukio la traffic anaburuzwa barabarani na bajaji China

on

Moja ya kazi ambazo ni za hatari sana duniani, kazi ya traffic nayo imo !! Barabarani kila mtu ana akili yake, nakumbuka moja ya matukio ya kusikitisha ambayo yalitokea Dar es Salaam March 2013 ilikuwa tukio la kugongwa kwa askari mmoja eneo la Bamaga ambapo mtu aliyegonga alikimbia huku akiongozana na gari za msafara wa Rais.

Nimekutana na hii video kwenye mtandao wa TV ya CCTV ambayo ni TV ya China… Askari inaonekana alisimamisha Bajaji alafu wakashindwana na dereva wa Bajaji hiyo, jamaa wa Bajaji akaiwasha kumkimbia askari huyo, lakini askari nae hakumwacha.. akaning’inia ubavuni huku Bajaj ikiendelea na safari yake..

Mwisho wa yote ilikuja gari moja ambayo ilikuja ikasimama mbele kuizuia Bajaji hiyo.

Video yote hii hapa, ikionesha tukio lote traffic huyo akiburutwa na Bajaj hiyo

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments