Ugonjwa wa corona umeendelea kushika kasi Duniani huku idadi ya vifo na wagonjwa ikiongezeka kila kunapokucha kwenye Nchi mbalimbali, Tanzania tayari imethibitisha kuwa na wagonjwa 12, Kenya 15 na uganda ni mgonjwa mmoja, lakini China ambako ugonjwa unaaminika kuanzia idadi ya vifo imefikia zaidi ya Watu 3000.
Janga la corona pamoja na mambo mengine, limethiri pia sekta ya uchumi hasa kwenye upande wa biashara, Soko la Kariakoo, DSM ndio kitovu cha biashara Tanzania lakini wafanyabiashara wanasema tangu kuzuka kwa janga la corona na Serikali kuwataka Watu kuepuka mikusanyiko, idadi ya wateja wanaofika kununua bidhaa imeshuka na kukwamisha biashara, lakini hata China ambako wanachukua bidhaa zao nako hakuendeki hivyo kuwalazimu kutumia mbinu mbadala ikiwemo kutumia mitandao kuuza na kununua bidhaa.