Top Stories

CORONA TANZANIA:Serikali yatoa maagizo ‘Muwe karibu na familia, wazee na watoto’

on

Wazazi na walezi nchini wametakiwa kufanya tathmini juu ya fursa na changamoto zilizopo katika familia zao hususani kipindi hiki ambacho jamii inakabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugojwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19).

Wito huo umetolewa leo jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza kuhusu Siku ya Familia Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 15 ya Mwezi Mei.

Waziri Ummy amesisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanatumia kipindi cha mapambano dhidi ya Corona kuwa karibu na familia zao huku wakifanya ufuatiliaji wa karibu hasa kwa watoto na Wazee kwa kufuatilia hali zao za lishe na endapo kuna mabadiliko wachukue hatua stahiki ya kutoa taarifa na kuwapeleka katika vituo vya kutolea huduma za Afya.

Waziri Ummy ameziasa familia zisiwanyanyapae waliopata maambukizi ya Corona tabia ambayo inaweza kupunguza upendo na utu miongoni mwa Watanzania wakati huu wa mapambano dhidi ya COVID-19.

“Niwaombe wazazi na walezi muwe karibu na familia zenu hasa watoto na wazee na punde mnapobaina dalili za ugonjwa wa Corona watoe taarifa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa”- Ummy Mwalimu

Soma na hizi

Tupia Comments