Israel imeweka masharti mapya kwa wiki tatu kukabiliana na mlipuko mpya wa ugonjwa wa COVID-19, ambao umeendelea kusambaa nchini humo.
Masharti hayo ya watu kukaa nyumbani yataanza kutekelezwa Ijumaa wiki hii, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameyasema hayo katika hotuba kwenye televisheni.
Katika kipindi hiki, ambacho kinaendana na wakati mgumu katika kalenda ya Kiebrania, watu watatakiwa kutembea hadi mita 500, isipokuwa kwenda mahali pa kazi, ambapo idadi ya wafanyakazi itapunguzwa.
Shule na vituo vya ununuzi vitafungwa, lakini maduka makubwa yatabaki wazi, kama vile maduka ya dawa. huduma za umma zitafanya kazi kwa idadi ndogo ya wafanyikazi na makampuni ya kibinafsi yataweza kuendelea kufanya kazi, kwa masharti ya kutopokea wateja.
“Ninajua kuwa hatua hizi zitatugharimu sana. Hizi sio aina ya sherehe ambazo tumezoea na hakika hatutaweza kuzisherehekea na familia zetu,” amesikitika Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye usimamizi wake dhidi ya mgogoro huo wa kiafya unapingwa.
Kulingana na Waziri wa Fedha, masharti haya mapya yatagharimu Euro Bilioni 1.6.