Top Stories

Corona yachochea ugomvi wa Marekani na Iran “Mmetengeneza corona, mnataka kutuua, tutalipa kisasi” (+video)

on

Kiongozi wa juu zaidi Iran ambaye pia ni Kiongozi wa Dini nchini humo Ayatolla Ali Khamenei ameishangaa Marekani kwa kitendo chake cha kutaka kuisaidia Iran kupambana na virusi vya corona na kusema Marekani ni waongo na wauaji.

“Marekani mara nyingi wamejaribu kuonesha nia ya kutusaidia inashangaza maana wenyewe wanateseka na Corona, tangu lini mfu akamzika mfu mwenzake, Marekani mnalaumiwa kuwa mmevitengeneza virusi hivi tutawaamini vipi?, sijajua kama ni kweli mmetengeneza ila kunapokuwa na tuhuma na maneno kama hayo, Mtu gani mwenye akili timamu atawaamini nyie?, mnaweza kujifanya mnaleta misada mkaishia kutuletea dawa zinazosambaza virusi au dawa zinazofanya corona ibaki milele”– AYATOLLAH

 

 

 

Tupia Comments