Michezo

Corona yaharibu program ya Lampard “Nashindwa kuwa-push”

on

Kocha wa club ya Chelsea ya England Frank Lampard ameeleza kuwa mlipuko wa virusi vya corona vimekuwa vikimletea wakati mgumu hata yeye katika kupanga program yake.

Lampard aeleza kuwa inamuwia wakati mgumu kuwasukuma wachezaji wake kufanya mazoezi wakati huu ambao hata yeye hajui ratiba ya kuendelea kwa EPL itakuwa lini.

“Ni ngumu sana kwa sasa kwa sababu hatujapata picha halisi ya kinachokuja mbele yetu (ratiba) inaonekana mambo yanaweza kubadilika kwa haraka tunaweza kwenda kwa na tarehe (kurudi kwa EPL) ila kwa sasa inaonekana kama May 1 hivi au April lakini tunafanyaje mazoezi sasa?”

Soma na hizi

Tupia Comments