Waziri wa Nishati, Dr.Medard Kalemani amesema Watanzania wasiwe na hofu ya ugonjwa wa CORONA kwani miongoni mwa Sekta iliyo imara ni ya Nishati ambapo tangu uwepo ugonjwa huo hakuna athari zozote.
Waziri Kalemani ameyasema hayo katika Bandari jijini Dar es Salaam wakati akifanya ukaguzi wa maeneo ya kupakua mafuta kutoka nje ya nchi.