Unaweza kuanza kujiuliza huyu jamaa alipataje ujasiri wa kushambulia na kuua ndani ya eneo la Mahakama?
Mwenyewe kasema kwamba alikuwa analipiza kisasi.. akafanya tukio hilo ambalo limechukua uzito wa juu kwenye habari kubwa leo DUNIANI !!
Anaitwa Claudio Giardiello, alifikishwa Mahakamani ya Milan, Italy jana ambapo akiwa katika ghorofa ya tatu ya Jengo la Mahakama hiyo alianza kushambulia kwa bunduki ambayo alikuwa nayo yeye mwenyewe.
Maafisa wa idara ya Mahakama wamesema mtuhumiwa huyo alikuwa na kesi ambayo ilitakiwa afilisiwe mali zake.
Mtuhumiwa aliwapiga risasi watu wawili ndani ya Mahakama na pia kumuua Jaji ambaye ilikuwa asikilize kesi yake.. mtu wa nne alifariki kutokana na mshtuko wa moyo kwenye eneo hilo.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alikamatwa umbali wa kama kilometa 30 toka eneo la Mahakama hiyo ambapo alitoroka akiwa na pikipiki.
Bado kuna maswali mengi.. Kwanza wanajiuliza jinsi ambavyo mtuhumiwa huyo aliweza kuingia na silaha eneo hilo la Mahakama ambalo lina ulinzi mkubwa.
Kingine ni kwamba wanajiuliza imekuwaje jamaa akajiamini na kufanya shambulizi kubwa kiasi hicho kwenye eneo la Mahakama.
Bonyeza play kuangalia video ya tukio hilo…
millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, movies, magazeti, video mpya na nyingine kubwa…. unaweza kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook