Vituko/ Comedy

Mahakama inafikishiwa kesi ya mwanaume aliyegoma kumtoa mke wake outing…

on

McDonaldsKesi imefika Mahakamani, mke anaomba mumewe ashitakiwe eti kosa ni kitendo cha mwanaume huyo kugoma kumtoa outing mkewe ili wakale chakula cha usiku katika mgahawa mkubwa town, ikaenda mbali zaidi pale mwanamke alipodai talaka.

Uttar Pradesh ni mwanamke aliyewasilisha madai hayo huko India dhidi ya mumewe Allahabad, ndoa yao ina miaka mingi ikiwa hai lakini kwa kosa hili la mume kumgomea outing mke wake kwenda diner kwenye migahawa mikubwa kama McDonald, tayari kumetia doa ndoa yao.

Jaji akaona isiwe tatizo, Mahakama ikakataa kusikiliza kesi hiyo na badala yake, Jaji akashauri wakamalizane kwa mshauri wa masuala ya ndoa.

Unadhani hii aliyofanya mwanamke huyu iko sawa mtu wangu? Nitafurahi ukiniandikia comment yako.

Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments