Stori Kubwa

Kwenye zile zilizoripotiwa leo Kenya ipo ya mauaji na pamoja na ubakaji wa watoto…

on

downloadMtu mmoja Nakuru nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 75 kwa kosa la kumbaka mtoto wake na kumuambukiza virusi vya HIV.

Taarifa zinasema kuwa mwanaume huyo Devid Waweru alifika nyumbani kwake usiku akiwa amelewa na kumkuta mtoto wake amelala, akamuamsha na kumbaka na kumuambukiza maradhi hayo.

Mwanaume mwingine amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumnajisi mtoto wake na kisha kumuua  baada ya kushinda naye Kanisani siku moja kabla ya kumfanyia kitendo hicho.

Unaweza kuisikiliza taarifa hiyo niliyoirekodi kutoka kituo cha K24 kwa kubonyeza play hapa.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments