Michezo

Baada ya stori za kuvunja mkataba wake, Andry Coutinho katua Dar, huu ndio msimamo wa Yanga (+Audio)

on

Headlines za usajili katika soka bado zinachukua nafasi katika dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, Kama utakuwa unakumbuka vizuri November 25 mkuu wa idara ya habari wa Yanga Jerry Muro alithibitisha kuwa mchezaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea klabu ya Dar Es Salaam Young African Andry Coutinho kavunja mkataba wake.

Kiungo huyo wa Brazil ambaye ameichezea Yanga toka akiwepo kocha wa kibrazil Marcio Maximo, aliingia katika headlines ya kuvunja mkataba na Yanga baada ya kusafiri kwenda kwao Brazil na kukaa kwa muda mrefu bila kuwa na taarifa yoyote rasmi kabla ya weekend hii kutua Dar Es Salaam akitokea kwao Brazil.

c019f54478646726dba553f996ddafcb

millardayo.com ilimtafuta katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha azungumzie kuhusiana na hatma ya Andry Coutinho ambaye anahusishwa kwa siku za hivi karibuni kumtemwa nyota huyo, Ni kweli wamemtema? mkataba wake vipi umevunjika?

“Ishu ya Coutinho ipo pande mbili anaweza akabaki Yanga au akaondoka, hii ni kwa sababu kuna klabu inamuhitaji, nani atakuwa mbadala wake? bado hatujui kwani hatuna uhakika kama ataondoka au la, Coutinho alikuwa Brazil kumuuguza bibi yake ambaye alikuwa anaumwa kansa na alimtibia na kuishiwaa hela ya tiketi, sisi alitutumia barua ilichelewa kufika baada ya kuipata tukamtumia tiketi” >>> Dk Tiboroha

Zaidi msikilize hapa katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments