Michezo

Zile goli 5 za Cristiano Ronaldo zilizomuweka kwenye HEADLINES kubwa unaweza kuzicheki hapa mtu wangu (VIDEO)

on

CR7

HEADLINES leo kuanzia kwenye TV kubwa duniani.. radio, magazeti.. mitandaoni.. ishu kubwa kwenye michezo ni ushindi wa nguvu waliopata Real Madrid..Ile Real Madrid VS Granada… matokeo yakawa 9-1.

Cristiano Ronaldo nd’o jina la mchezo, kwenye hizo goli 9 zake pekeake  ziko 5 yani.. labda hukumuona jamaa akiyapachika hayo magoli 5 wavuni.. nakusogezea kipisi cha hii video uone hizo goli zote Ronaldo alivozisogeza wavuni mtu wangu.

https://www.youtube.com/watch?v=mFVocCnEltg

Ronaldo anaendeleza ukali wake, ana jumla ya magoli 47 katika mechi 11, watu wakamlinganisha na Messi eti.. yeye ana goli 43 katika mechi 41.. Ronaldo yuko kifua mbele kwa goli nne mtu wangu.

Kaa karibu na millardayo.com nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments