Michezo

Ronaldo amejibuje alipoulizwa kama atahudhuria Ballon d’Or? na akishindwa je?

on

ronaldo 3October 2013 Rais wa FIFA Sepp Blatter aliomba radhi na kusema maneno aliyoyasema hayakua na lengo la kumshushia heshima au kumdharaulisha mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Blatter kwenye mazungumzo na Wanachuo wa Oxford Uingereza alisema mchezaji Messi ni kama Mtoto mtiifu anamvutia mtu yoyote ambaye ni mzazi na hana makuu na sio kama Ronaldo ambae huwaamrisha wenzie uwanjani kama inavyokuwa vitani,  anatumia fedha nyingi kwa ajili ya masuala ya urembo hasa nywele zake’

Hii ni kauli ambayo haikumpendeza Ronaldo ambae aliishia kurusha dongo kupitia facebook page yake kwa kusema “namtakia Blatter afya njema na maisha marefu ili aweze kuwashuhudia wachezaji anaowapenda na timu anazopenda zikipata mafanikio’

ronaldo 5Mpaka sasa kumeonekana kama sio shwari kihivyo kati ya Ronaldo na Blatter ambapo kuna kipindi zilisambaa sana stori kwamba Ronaldo hana mpango na tuzo za Ballon d’Or zitakazotolewa hivi karibuni.

Hili ndio jibu alilotoa baada ya kuulizwa kama atahudhuria utoaji wa tuzo hizi 2014 >>> ‘nimeshafunga mjadala kuhusu hii ishu na sitaki kuizungumzia tena, naweza kusema tu kwamba nitahudhuria utoaji wa hii tuzo, kama nikishinda itakua poa sana na kama sitoshinda basi maisha yataendelea’

Screen Shot 2014-01-08 at 9.26.49 PM

Tupia Comments