Michezo

Sasa hiki ndicho alichokisema Ronaldo kuhusu ripoti za kumtukana Messi

on

Screen Shot 2014-11-12 at 5.58.43 PMJana Jumanne gazeti la Daily Telegraph liliandika habari ya kusisimua kutoka kwenye kitabu cha mwandishi wa SKY Sport Guillem Balague kiitwacho “MESSI” ambacho kiliandika >>> “Ronaldo, labda kwa dalili za kuwa na akili za kitoto ambazo wanazo wacheza soka wengi, anadhani kwamba kuna ulazima kujitamba mbele ya wachezaji wenzie, akionyesha hamuogopi Messi na yupo tayari kushindana nae’

Ndio maana kwa mujibu wa baadhi ya wachezaji wa Real Madrid, CR7 amekuwa akimpa Messi majina ya ajabu kwa kumuita  ‘motherf—-r’ na pale anapomuona mchezaji yoyote wa Real Madrid akiongea na Leo Messi, basi nae huishia kumuita (tusi) ‘motherf—-r’.”

Taarifa hii ya Balague ilitengeneza vichwa vya habari vingi kwenye media na haikumchukua Ronaldo muda mrefu kujibu shutuma hizo kupitia mashabiki wake millioni 100 kwenye mtandao wa Facebook.

Pamoja na kukanusha taarifa kumtukana Messi, Ronaldo amesisitiza kwamba amempa Mwanasheria wake ruhusa ya kuchukua hatua za kisheria juuy a mwandishi huyo huku akisema anawaheshimu Wanasoka wote na Messi akiwemo.

Screen Shot 2014-11-12 at 6.02.04 PM

 

Tupia Comments