Wananchi wa Wilaya ya Manyoni wameomba serikali ingilie kati baada ya mauaji yanayotokea katika eneo hilo huku wakiomba ulinzi uzidishwe zaidi hasa kutoka jeshi la Polisi.
Wananchi hao wameomba wakati wa Mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo na kusema kwasasa wanakosa amani kwani hawajui nani anafata katika kuwawa hivyo uchunguzi wa kina ufanyike.
Akitolea ufafanuzi hoja hiyo Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameeleza kua mauaji mengi ya wilaya ya Manyoni niya kishirikina na ameunda tume inayoshirikisha vyombo vya ulinzi vyote ambayo ipo inaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha mauaji hayo
“Katika zoezi hili ambalo tunaendelea nalo kila ambaye atashukiwa akiendesha mambo haya atutakuwa na mswalia mtume”
Jambo lingine lilikua linatokea hospital mtu anatokea amefariki amepelekwa monchwari wanakwenda kuondoa baadhi ya viungo yote haya tunaendelea na uchunguzi tutawabaini wote wanaohusika” RC Singida