Stori Kubwa

Pale ambapo ushirikina umehusishwa kwenye mauaji ya watu hawa mkoa wa Mara..

on

crime-intelligence

JESHI la Polisi Mkoa wa Mara limewakamata watu  saba wakiwemo viongozi wawili wa Serikali ya kijiji cha Park Nyigoti, wilaya ya Serengeti baada ya kutuhumiwa kuwakamata na kuwafunga vitambaa usoni watu nane wanaowatuhumu kwa uchawi kisha kuwachapa viboko na kusababisha vifo vya watu watano.

Kaimu Kamanda wa Polisi na kamishina msaidizi wa Jeshi la Polisi ACP Ernest Kimola, amesema tukio hilo limesababisha  watu  wengine watatu kujeruhiwa kwa viboko na kulazwa katika Hospitali teule ya Nyerere DDH mjini Mugumu, mbali na mwenyekiti na mtendaji viongozi wawili wa jadi wamekamatwa wakihusishwa na mauaji hayo.

Wananchi  hao walikamatwa katika miji yao kisha kufunga vitambaa usoni na kuchapwa viboko hadi kufa kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya ushirikina, viongozi hao wa jadi  kwa kushirikiana na Serikali  ya kijiji waliitisha mkutano kwa lengo la kuwabaini watu wanajihusisha na ushirikina ambao  umesabisha mvua  kutonyesha kijijini hapo  ambapo  watu wanane  walitajwa  katika  mkutano  huo.
Kaimu Kamanda huyo amewasema tukio hilo lililotokea alfajiri March 2 na kisha miili ya waliouawa ikitupwa karibu nyumba zao huku watu wengine watatu wakilazwa Hospitali kutokana na majeraha ya kupigwa.
CHANZO: Habari ITV March 05, 2015
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments