Michezo

Cristiano Ronaldo apata Corona

on

Staa wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amepimwa na kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona, Ronaldo ameondoka katika kambi ya Ureno na kujitenga.

Chama cha soka Ureno kimethibitisha kuwa Ronaldo ana maambukizi ila hana dalili yoyote, wachezaji wenzake wote wamepimwa hawana na wako tayari kwa mchezo dhidi ya Sweden wa National League utakaochezwa Jumatano hii.

Kwa sasa Ronaldo amejitenga na anaendelea vizuri sambamba na kufuata na kuzingatia miongozo ya wataalam wa afya, baada ya Ronaldo kukutwa na maambukizi wenzake walipimwa tena na kukutwa negative.

Soma na hizi

Tupia Comments