Michezo

Achana na headlines za Ronaldo kuvunja rekodi yake ya UEFA, hizi ndio rekodi zake 10 za soka zinazo sisimua …

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, usiku wa December 8 katika mchezo dhidi ya Malmoe FF wa kuhitimisha mechi za Makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alivunja rekodi yake mwenyewe aliyoiweka msimu uliyopita, kabla ya mchezo huo uliyomalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 8-0, Ronaldo alikuwa anashikilia rekodi ya kuongoza kwa kufunga magoli mengi katika mechi za Makundi, kwani alifunga magoli 9 msimu uliyopita.

Usiku wa December 8 aliingia uwanjani akiwa tayari kafunga jumla ya magoli 7 katika mechi 5 zilizopita za hatua ya makundi, hivyo kufunga kwake goli nne katika mchezo dhidi ya Malmoe FF kulimfanya afikishe jumla ya magoli 11 na kuvunja rekodi yake ya msimu uliyopita, rekodi ambayo hakuna mchezaji aliyekuwa kaifikia. Mtu wangu wa nguvu hiyo sio rekodi ya kwanza ya Ronaldo, naomba nikusogezee rekodi 10 kali za Ronaldo.

1- Wakati akicheza Man United Ronaldo alifanikiwa kuvunja rekodi ya mkongwe wa timu hiyo George Best ya ufungaji wa magoli 33 katika msimu wa 1967/1968 na kumfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza wa Ureno kucheza kwa mafanikio Man United.

epa04477463 Real Madrid's Portuguese forward Cristiano Ronaldo gives thumbs up after receiving the Golden Boot award as top scorer in all European soccer leagues of the 2014-2015 season during a ceremony in Madrid, Spain, 05 November 2014. Cristiano also won the Golden Boot award in the 2007/2008 and 2010/2011 seasons. EPA/JUAN CARLOS HIDALGO

2- Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi kubwa za Ulaya kufunga magoli 50 na zaidi katika msimu mmoja. rekodi ambayo aliiweka kwa kufunga magoli katika mashindano matano tofauti.

3- Staa huyo pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 100 ya Ligi katika kipindi kifupia, kitendo ambacho kimemfanya kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufanya hivyo, Hata hivyo magoli hayo yalimfanya Ronaldo kuwa mchezaji wa kwanza wa Laliga kuzifunga timu zote 19 za Laliga zilizocheza dhidi ya Real Madrid.

4- Ronaldo anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga magoli 17 katika msimu mmoja wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifanya hivyo katika msimu wa 2013/2014.

Cristiano-Ronaldo-is-Now-Tenth-Top-Scorer-in-La-Liga-History

5- Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 200 za haraka za Laliga katika jumla ya michezo 178 December 2014. Alifunga hat-trick dhidi ya Celta Vigo na kufikisha jumla ya hat-trick 23 zilizoingia katika rekodi ya Laliga.

6- Ronaldo alifunga jumla ya hat-trick 8 katika msimu mmoja wa 2014/2015 na kuweka rekodo ya kufunga hat-trick nyingi zaidi kuwahi kufungwa katika msimu mmoja wa Ligi.

7- Aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Sporting Lisbon kucheza katika vikosi vya (U-16), (U-17), (U-18), timu B na kikosi cha kwanza cha kwanza cha Sporting Lisbon yote hiyo amecheza katika msimu mmoja.

ronaldoget_2327179b

8- Wakati anacheza Man United Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu wa Ligi Kuu Uingereza kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi mara mbili mfululizo, alifanya hivyo mwaka 2006 kwa kutwaa tuzo hiyo mwezi November na December. Wengine waliowahi kufanya hivyo ni Robbie Fowler mwaka 1996 na Dennis Bergkamp mwaka 1997.

9- Ronaldo ni mchezaji wa pili kutwaa tuzo ya Ballon d’Or mara nyingi, ametwaa mara tatu mwaka 2008, 2013 na 2014, anayeongoza kwa rekodi hiyo ni Lionel Messi aliyetwaa mara nne.

cristiano-ronaldo-ballon-2014

10- Ronaldo ndio mchezaji wa kwanza Ligi Kuu Uingereza kuwahi kutwaa tuzo nne za PFA na FWA kwa msimu mmoja, Ronaldo alifanya hivyo mwaka 2007 akiwa katika klabu ya Man United.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments