Michezo

Hii ndio zawadi ya harusi ambayo Cristiano Ronaldo kaamua kumnunulia wakala wake…

on

Ni zawadi gani ya ndoa unaweza kumnunulia wakala namba moja wa wachezaji duniani?

‘Super agent’ Jorge Mendes, wakala wa Jose Mourinho, James Rodriguez, Nani, Falcao, Angel Di Maria, Cristiano Ronaldo, anatarajia kumuoa mchumba wake wa siku nyingi, Sandra Barbosa Ureno.

Cristiano Ronaldo, ambaye ni mteja mkuu wa Mendes, atakuwa ‘best man’ katika harusi hiyo, na taarifa kutoka Ureno zinasema mshambuliaji huyo wa Madrid anatarajia kumpa zawadi ya kisiwa atakachomnunulia Ugiriki.


Habari za Ronaldo kumzawadia Mendes zilianza kuripotiwa na mtandao wa Noticia.

Kwa mujibu wa ripoti, Ronaldo anatarajia kutumia Pound Milioni 50 kwa ajili ya kununua kisiwa hicho.

Mendes sio jamaa ambae ana maisha ya kikawaida kabiisa, utajiri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya Pond Milioni 100 hivi.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments