AyoTV

Video: Vitendo vinavyoendelea Zanzibar vimeigusa CUF, na haya ndio maamuzi yao…

on

March 17 2016 Chama cha Wananchi CUF kilijitokeza  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam kupitia Naibu katibu Mkuu Magdalena Sakaya kuitaka Serikali iingilie kati vitendo vinavyofanywa na watu wanaojiita ‘mazombi’ kwa kuwapiga wananchi na wafuasi wa chama hicho, aidha wamewashutumu polisi kwa kuwashikilia viongozi wa chama hicho bila sababu…

Kumekuwa na vikundi viovu vikiwavamia wafuasi wa CUF na kuwapiga pamoja na kuwajeruhi, maarufu kwa jina la mazombi jeshi la polisi mpaka leo hii hawajakamata Zombi hata mmoja na wanasema kwamba hao mazombi hawawajui na hawapo, lakini cha kushangaza kila tukio baya likitokea Zanzibar wanasingiziwa wafuasi wa CUF‘ :-Magdalena Sakaya

kila siku viongozi wa CUF wanakamatwa na mpaka hivi sasa wafuasi wa CUF zaidi ya 60 wamekamatwa wakisingiziwa kuhusika na uvunjifu wa amani‘ :-Magdalena Sakaya

 

 Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments