Juzi April 22 2017 watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Prof. Ibrahim Lipumba walivamia mkutano wa wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad na kuwajeruhi wenzao pamoja na waandishi wa habari.
Leo April 24 2017 Serikali imetoa taarifa kuhusu tukio hilo ambapo Mkurugenzi, Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amesema: “Tumechukua muda kidogo kulifuatilia suala hili na kubaini licha ya baadhi ya waandishi kujeruhiwa na kuripoti polisi, wapo ambao vifaa vyao vya kazi vililengwa katika shambulizi hilo.
“Ifahamike kuwa uandishi wa habari ni taaluma adhimu na nadhifu inayopaswa kuheshimiwa, kuenziwa, kulindwa na kutoingizwa katika migogoro ya pande zinazofarakana katika jamii.” – Dkt. Hassan Abbas.
VIDEO: Tukio la uvamizi kwenye mkutano wa CUF Dar es Salaam, Bonyeza play hapa chini kutazama