Habari za Mastaa

Cardi B aeleza chanzo cha kumvamia Nicki Minaj

on

Baada ya Cardi B na Nicki Minaj kutaka kuzichapa kwenye sherehe ya ‘Harper’s Bazaar’ New York usiku wa September 7,2018 kwa mara ya kwanza Cardi B amefunguka kuhusiana na sakata hilo la kumvamia Nicki Minaj.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya Cardi B na W Magazine ameeleza na kusema kuwa aliwahi kuzungumza na Nicki Minaj mara mbili na waliyamaliza lakini amesema kuwa kwa upande wa Nicki Minaj ameendelea kumuongelea vibaya.

Inaelezwa kuwa kitu ambacho kimemuumiza zaidi Cardi B ni ‘like’ ya Nicki Minaj kwenye mtandao wa twitter inayosema kuwa hajui kumlea mtoto wake Kulture na alishangazwa na like hiyo kwa mtu ambaye hana hata mtoto kufanya hivyo.

“Kwa muda sasa amekuwa akinirushia maneno na niliongea nae kama mara mbili na tukaelewana, lakini aliendelea mimi ni mama mzuri na najua kulea” >>>Cardi B

Nicki Minaj aliwahi kukanusha kuhusiana na taarifa hizo kupitia radio yake ya “Queen’s Radio” na kusema kuwa hajawahi kumuongelea mtoto wa mtu yoyote vibaya na wala kuongelea kuhusu matunzo .

Baba wa MO DEWJI “ni kweli Mwanangu ametekwa”

Soma na hizi

Tupia Comments