Top Stories

Katibu Mkuu mpya CUF “Waliochoma bendera na kufuta rangi zetu tumefungua kesi”

on

Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Wananchi CUF Khalifa Suleiman Khalifa akiongea na Waandishi wa habari amesema Chama hicho tayari kimefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Vuga kwa wale waliohusika na kuchoma bendera, kufuta rangi za CUF na waliopachika bendera za ACT katika Ofisi zao.

Namnukuu “Tumekusanya ushahidi wa yote yaliyofanyika, majina ya waliofanya vitendo vya kufuta rangi za Chama chetu, waliochoma moto bendera zetu, waliopachika bendera za ACT isivyokuwa halali ktk Ofisi zetu, ushahidi umekamilika, tumefungua kesi ktk Mahakama Kuu ya Vuga” Katibu Mkuu CUF

Taarifa hii ya Katibu Mkuu Khalifa imetokea kukiwa na mvutano katika ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Chama cha ACT Wazalendo juu ya matuko hayo.

LIVE: ZITTO KABWE AJIBU ISHU YA MSAJILI KUTAKA KUKIFUTA CHAMA CHA ACT WAZALENDO

Soma na hizi

Tupia Comments