Siku mbili baada ya kifo cha mwanafunzi na kiongozi wa wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Meru nchini Kenya Evans Njoroge kimefungwa kwa muda usiojulikana.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye vyombo vya habari nchini humo, Katibu wa Baraza la Mawaziri Amina Mohamed, ameeleza kuwa ameunda timu ambayo itafanya uchunguzi wa kutafuta sababu ya kifo cha mwanafunzi huyo.
Inaelezwa kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kupigwa na risasi na polisi siku ya Jumanne February 26, 2018 wakati wa maandamano ya wanafunzi ambayo yalisababisha vurugu kubwa.
Marehemu Evans alipigwa risasi na askari wakati akiongoza maandamano hayo ambayo yalikuwa yakipinga kile walichodai ni kunyanyaswa na Makamu Mkuu wa chuo hicho huku wakishinikiza ajiuzulu haraka.
Madiwani wawili wa CHADEMA wajiuzulu Serengeti kuhamia CCM
Nyimbo 13 za Bongofleva, TCRA imeagiza zisipigwe Redioni wala TV