Michezo

Simba SC safari hakuna tena, UD Songo kaharibu mipango

on

Club ya Simba SC leo ilicheza mchezo wake wa marudiano wa kuwania kufuzu kucheza hatua ya Makundi ya CAF Champions League dhidi ya club ya UD Songo kutokea nchini Msumbiji.

Mchezo wa kwanza nchini Msumbiji ulimalizika kwa 0-0, hivyo game ya marudiano uwanja wa Taifa Simba SC wametoka sare ya kifungana goli 1-1, hivyo licha ya kufanana lwa idadi ya magoli lakini Simba anatolewa kwa goli la ugenini.

Goli la UD Songo lilifungwa na nahodha wao Luis Miquissone dakika ya 13 ila Simba SC walisawazisha kwa penati dakika ya 86 kupitia kwa Erasto Nyoni, Simba SC kutokana na kutolewa round ya awali haendi popote tofauti na Yanga ambao hata wakitolewa round inayofuata wanaenda kucheza Kombe la shirikisho.

Soma na hizi

Tupia Comments