Mix

Young Dee athibitisha kufanyiwa uhalifu na Van Damme wa Sinza

on

Unakumbuka Hekaheka ya CloudsFM iliyoruka January 19 2017 kwenye LEO TENA ikihusu mitaa ya Sinza makaburini Dar es salaam na mtu anakosesha watu amani?

Ni jamaa ambae amekuwa akifanya matukio ya uhalifu ikiwemo kuchukua mali za watu kibabe kama vile simu na anajulikana kwa jina la ‘Van Damme’, Wananchi wa eneo hilo wamesimulia kuwa ‘Van Damme’ akifika maeneo hayo maduka yanafungwa na madereva bodaboda wanamkimbia.

Kupitia Instagram Young Dee kathibitisha kukutana na Van Damme wa sinza anayepora watu na kuibiwa vitu vyake mbali mbali ikiwemo simu yake ya mkononi, pochi na vitu vingine.

Young D aliandika >>> “Usiku wa kuamkia juzi tulivamiwa na jamaa anaesemekana ni Dame wa sinza nikiwa nmekesha studio maeneo ya Sinza Palestina kwa Mr T touch, sasa juhudi za kumpata zimekua ngumu maana amekua na matukio ya hivyo mara kwa mara”

Juzi kaiba simu mbili moja ni yangu (iphone6s+) na Samsung na wallet yangu iliyokua na vitambulisho vyangu pamoja na kadi ya bank, sasa kwa yoyote ataepata taarifa itayoweza kunisaidia naomba anifate Dm tafadhali! ? Tag wana wote wa sinza tusaidiane kwa hili

HEKAHEKA: Scorpion mwingine aibuka Sinza, anajiita Van Damme… bonyeza play kwenye hii video hapa chini

Soma na hizi

Tupia Comments