Habari za Mastaa

“Siku mkiniona VEVO basi mjue nimeyakamilisha haya” – Diamond Platnumz

on

Awali msanii wa Bongofleva Diamond platnumz hakuwepo kwenye Mtandao maarufu wa kuweka video (VEVO) na alipoulizwa alijibu kuwa uwepo wa msanii Vevo anatakiwa alipwe zaidi ya anavyolipwa kwenye upande wa Youtube.

Baada ya kujiunga Vevo Diamond February 26 ameyaandika yafuatayo >>>”Kuna siku niliulizwa kwanini we haupo vevo… nikawambia uwepo wa msanii @VEVO anatakiwa msanii alipwe zaidi ya alivyokuwa analipwa kwenye Youtube channel ya kawaida”

“Vevo wenyewe pia wamtambue kuwa kuna msanii anaitwa Nasibu Abdul aka Diamond toka Tandale, na pia anacholipwa msanii wa Marekani kwa view moja ama tangazo lolote liekwalo mwanzo ama lipitalo katikati pindi ya utazamaji wa video hiyo basi nae anapaswa kulipwa hivyohivyo”

“Mbali tu ya kumlipa, VEVO yapaswa kwa namna moja au nyingine kusaidia kupromote maana ni biashara yao wote na kila msanii ana shabiki zake na ukubwa na nafasi yake atokapo” hivyo nikawambia: “siku mkiniona nipo vevo basi jua nimeyakamilisha haya, vinginevyo wacha niendee kuokota senti mbili tatu, kwenye chanel yangu ya Youtube kawaida.

SABABU YA KUYASEMA HAYA:

Ni kutaka kuwafahamisha ama kuwaamsha baadhi ya wasanii wenzangu watambue kuwa
Mziki wetu hata kama hauko mkubwa saaaana ulimwenguni, ila Mwenyez Mungu kausaidia kuufikisha sehem flani, hivo wasanii lazma tujitambue na Tuwe na Misimamo na kazi zetu.

Vilevile umakini kwenye maamuzi ama hatua yoyote tutayoichukua juu ya sanaa zetu kwa sasa maana tuliamualo leo linaweza kutujenga ama kutubomoa baadae… nafahamu Wasanii wengi hawakuwa wakilifahamu hilo na badala yake kuingia @VEVO kupitia watu kati ama madalali na kuambulia status mtaani kuwa wako @VEVO ilhali nyuma kuna watu wanawadhurumu mamilioni ya pesa zitokanazo na jasho lao…”

kwa uchungu wa kufaham namna gani inauma msanii ukinyonywa kazi yake ndio umenifanya nilizungumze hili leo, ila ukiona kwa namna moja au nyingine nimekosea Tafadhali mnisameh…? -SIMBA #MALENGO

VIDEO: Polisi yaongea kwanini Diamond Platnumz hakufikishwa Mahakamani kama wale wa Singida

Ulipitwa na VIDEO ya Zari na Diamond walivyotunzwa 40 ya Nillan na Zari alivyocheza vigoma

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako Millard Ayo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID NA IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments