Top Stories

Onyo alilotoa Waziri Ndalichako “Ukienda kwa michepuko yako utakiona”

on

July 19, 2018 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako kwa niaba ya Serikali amekabidhi magari 47 kwa ofisi za uthibiti ubora wa shule za kanda na Wilaya pamoja na baraza la mitihani Tanzania kwajili ya kusaidia  kuongeza ubora wa elimu nchini.

Prof Ndalichako amesema…>>>“Haya ni magari kwa ajili ya ufuatiliaji wa elimu na ninaagiza kwamba yasitumike tofauti na masuala ya elimu, yeyote atakayeenda kinyume kibarua chake kimeota nyasi.

Madereva mtakaokabidhiwa haya magari ni moto msije mkacheza nayo, isiwe umetumwa kwenye kazi wewe unaenda kwa michepuko yako. Utakiona cha mtemakuni” –Prof Joyce Ndalichako

“Mwanzo nilijutia, Makonda alijaribiwa ili awe mfano”–MC PILIPILI

 

Soma na hizi

Tupia Comments