Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro Dkt Hawa Ngasongwa amewataka akinamama wajawazito Kuzingatia Lishe Bora ambayo itasaidia Mtoto kuzaliwa akiwa na afya njema pamoja na uzito uliotimia.
Dokta Ngasongwa ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi jengo la wodi ya watoto njiti lilojengwa na shirika la SolidarMed kushirikiana na hospitali hiyo ambalo limegharimu zaidi ya Milioni 75.
Anasema hospitali hiyo wanazaliwa zaidi ya watoto elfu Saba Kwa mwaka ambapo Kati yao Mia moja Hadi Mia Mbili wanakuwa na uzito pungufu(Njiti) na kupelekea kulazwa hospitali hapo hadi pale Afya zao zitakapoimarika.
Anasema Ukosefu wa lishe Bora Kwa mama mjamzito imekua Chanzo cha watoto kuzaliwa chini ya uzito pungufu (njiti) hivyo mlo kamilo na matunda ni Muhimu Kwa akina mama Wajawazito.
Aidha Dokta Hawa anasema magonjwa ya presha pamoja na unywaji wa pombe nao unachangia kuongezeka Kwa changamoto hiyo kutokana na kumuathiri Mtoto aliyopo tumboni.
Kwa Upande wake Mkurugenzi mkazi shirika la SolidarMed lenye Makao makuu yake mjini Ifakara Wilaya ya Kilombero mkoani hapa bwana Beatus Saambili anasema Ujenzi wa jengo hilo ni mwendelezo wa hatua za kuunga mkono juhudi za Serikali Utoaji huduma bora za afya hasa mama na mtoto.
Anasema licha ya kushiriki katika Ujenzi lakini pia wametoa Mafunzo Kwa wataalam wa afya wa wodi hiyo namna ya utekelezaji wa majukumu yao.
Jengo hilo limegharimu zaidi ya milioni 70 na linauwezo wa kukaa vitanda 20 ambapo upatikanji wake umekua mkombozi hospitalini hapo.