Mwanamke mmoja tapeli huko Florida amekamatwa baada ya kushtakiwa kwa kumshawishi mwanamke aliyekiwa mteja wake kumlaghai mumewe tajiri dola milioni 1.
Wasso alikutana na Halfon mnamo 2017 wakati aliripotiwa kupitia wakati mgumu maishani mwake na akamwambia anahisi “giza” kutoka kwake na inaonekana alimwambia Halfon kwamba alikuwa na laana ya familia na ndipo alipoanza kumtibu kwa njia za jadi za uongo.
Ndipo 2018, Jaycee Wasso alidaiwa kumshawishi mteja wake Lin Halfon kuiba pesa kutoka kwenye akaunti ya mumewe mwenye umri wa miaka 80 kulingana na MEAWW,
Halfon alimpatia pesa kwa matumaini kwamba angeweza kuondokana na laana ya familia kwa kutumia uchawi na kuondoa roho zisizohitajika.
Lakini waendesha mashtaka walisema kulikuwa na ushahidi kwamba Wasso alimdanganya Halfon ili kumpa pesa na kutumia mbinu za kumtisha kuwa angesimamisha huduma ya kumtolea nguvu za giza kwake.
Baadhi ya meseji alizotumiwa na Wasso kwa Halfon alisema zilimtia hofu
“Lin, mizimu wanataka nikuambie kinachoendelea. Mama yako atakufa utapoteza kila kitu utapelekwa mbali unaenda gizani Giza litakuja kukushika.”
Halfon alitoa ushahidi mahakamani Jumanne kwamba hakuamini katika mizimu.
Sasa Wasso anakabiliwa na ulaghai, utakatishaji fedha, na mashtaka makubwa ya wizi wa magari huku halfon akifukuzwa nchini Israeli baada ya kutumikia kifungo cha miezi 13 kwa kuiba vito na pesa kutoka kwa mumewe pamoja na kuchukua dola milioni kwenye akaunti ya benki ya mume wake wa wakati huo, Richard Rappaport.