Habari za Mastaa

Cheki daladala hizi mbili zilizoamua kusambaza upendo na Serengeti Fiesta Tanga 2014

on

2hcStori za kuandikwa kwa majina ya wasanii na watu maarufu kwenye daladala mbalimbali Tanzania tumekua tukizisikia na kuzisoma sehemu mbalimbali,kuna ambazo zipo Dar,Arusha,Mwanza,Mbeya na miji mingine inayotumia usafiri huu.

Tangu nimeingia Tanga 96.0 miongoni mwa vitu nilivyovutiwa navyo ni pamoja na hizi daladala 2 ambazo zinafanya safari zake kati ya Pongwe na Stand,daladala hizi moja imeandikwa Sambaza Upendo nyingine imeandikwa Nishida.

Kimsingi hizi ndizo kauli mbiu za Fiesta 2014 lakini nilichokiona hapa ni namna watu hawa walivyoshawishika kuandika kwenye magari yao nilipata nafasi ya kuongea nao,mmoja wao ambaye ameamua kujipa la Fiesta Boy amesema kuwa anaipenda sana Clouds.

Ukitoa sababu hiyo pia kasema ni mhudhuriaji pia wa matamasha ya Fiesta kila mwaka ambapo kwenye gari yake ndani anayo karatasi ya Fiesta ya mwaka 2012 ambayo ilikua na kauli mbiu ya Bhaaaasi.

Jamaa kasema mazingira ya kazi yanawafanya saa zingine wapigane bao kwa sababu wanaenda njia moja lakini wana furaha kubwa kuona wote wanasambaza upendo na wanapiga kazi pamoja.

3hc

6hc

5hc

4hc

 

Tupia Comments