Mshambuliaji wa Barcelona, Dani Olmo, atakosa kucheza kwa takriban wiki tano baada ya kuumia misuli ya paja la kulia, klabu hito ya LaLiga ilitangaza leo Jumatatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alipata maumivu ya misuli baada ya kufunga goli katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Girona siku ya Jumapili na alitolewa uwanjani katika dakika ya 61.
Jeraha la Olmo ni pigo kwa kocha Hansi Flick, wakati timu yake inapoanza kampeni ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Alhamisi hii, baada ya kuanza vyema kwenye ligi ya ndani.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Hispania, aliyesajiliwa kutoka RB Leipzig kwa Euro milioni 55 (Dola 61 milioni), tayari amefunga magoli katika mechi zote tatu alizocheza kwa Barcelona msimu huu.
Klabu hiyo ya Catalonia itakutana na AS Monaco kwenye uwanja wa Stade Louis II Alhamisi, kabla ya kukabiliana na Villarreal kwenye mechi ya LaLiga siku ya Jumapili.