Michezo

Daniel Ek akanusha taarifa kuwa hajaomba kuinunua Arsenal

on

Bilionea wa Sweden na muanzilishi mwenza wa mtandao wa Spotify Daniel Ek (38) ameamua kutolea ufafanuzi kuhusiana na taarifa zilizoripotiwa leo kuwa hajatuma ofa ya kutaka kuinunua club ya Arsenal ya England.

“Taarifa mbalimbali leo zimesema kuwa sijatuma ofa ya kutaka kuinunua Arsenal, nafikiri ni muhimu kuweka rekodi sawa, wiki hii ofa ilitumwa kote kwa Joash Kroenke (mmiliki wa Arsenal) na watu wa Bank wanaomiliki hisa za mashabiki”

“Katika majadiliano na bodi walijibu kuwa hawahitaji pesa, naheshimu maamuzi yao lakini nabakia bado na dhamira ya kuinunua (Arsenal)”

Daniel Ek aliyedaiwa kutuma ofa ya Pound Bilioni 1.8 (Tsh Trilioni 5.8) kuinunua Arsenal, ameamua kuweka wazi suala hilo kupitia twitter account yake baada ya Club ya Arsenal kukanusha taarifa kuwa Daniel hajatuma ofa hiyo.

Soma na hizi

Tupia Comments