Moja ya habari iliyokamata headlines hii leo ni pamoja na kuanguka kwa Daraja kuu la ‘Francis Scott Key’ lililopo jijini Baltimore, katika jimbo la Maryland nchini Marekani baada ya kugongwa na meli ya mizigo iliyobeba kontena.
Zaidi ya watu 20 wanaripotiwa kuwa majini kulingana na taarifa kutoka kwa mamlaka ya Zima moto ya mjii wa Baltimore, na juhudi za uokoaji zinaendelea.
Msemaji wa mamlaka hiyo alisema walipokea simu kupitia huduma ya dharura ya 911 majira ya saa 1:30 usiku kuhusu ajali hiyo.
Shirika la habari la Associated Press wameripoti kuwa magari kadhaa yameanguka katika mto baada ya ajali hiyo.
Daraja hilo ni kilometa 2.5 ni kiungo muhimu kwa Watumiaji mbalimbali wa eneo hilo ambapo meli hiyo inayopeperusha bendera ya Singapore imetajwa kuwa na urefu wa futi 948 kwenda juu.
Mji wa Baltimore uliopo ndani ya Jimbo la Maryland ni mji wenye Wakazi zaidi ya laki tano kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2020 na ni nyumbani kwa Mastaa maarufu duniani kama Jada Pinkett Smith, Sisqó, Mwimbaji Marioo na aliyekuwa Spika Nancy Pelosi.