Top Stories

Maafisa wakuu sita wa ANC wanakutana na Zuma leo

on

Leo February 5, 2018 Maafisa sita wenye nguvu katika chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress – ANC watakutana  na Rais wa nchi hiyo Jacob Zuma, wakati shinikizo likiongezeka kumtaka kiongozi huyo anayezongwa na kashfa kuondoka madarakani.

Zuma amekuwa katika nafasi ndogo baada ya kukabidhi wadhifa wa Mwenyekiti wa chama kwa makamu wake, Cyril Ramaphosa. Mkutano kati ya vigogo sita wa ANC na Rais Zuma umetangazwa na katibu mkuu wa chama hicho, Ace Magashule, ambaye hata hivyo ameongeza kuwa suala la kumuondoa Zuma madarakani halipo kwenye ajenda ya mkutano.

Kauli yake imetofautiana na taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Afrika Kusini ikiwa ni pamoja na City Press na gazeti la Sunday Times, ambavyo vimenukuu chanzo ambacho hakikutajwa jina, kilichosema kuwa maafisa wakuu wa ANC watamtaka Zuma kujiuzulu.

JPM KWENYE SHEREHE ZA KUMUWEKA WAKFU ASKOFU JACKSON SOSTHENESI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments