Habari za Mastaa

Davido akana tuhuma za kula bata na Mama mtoto wake Ghana

on

Msanii wa Nigeria Davido amejitokeza kukana tuhuma zinazodai alikuwa akila bata Ghana na mwanamke aliyezaa naye baada ya kuonekana wakiwa wote kwenye private Jet yake wakielekea ghana, Davido amejitetea kwa kusema kuwa Mama wa mtoto wake alikuwa akienda Ghana kwaajili ya biashara zinazomuhusu mtoto wao hivyo akampa lifti kwenye Jet yake kwakuwa na yeye alikuwa akienda huko huko.

Davido ametoa ufafanuzi huo baada ya watu kumshtumu kwenye mitandao ya kijamii ambapo yeye ameeleza kuwa hajapendezwa na swala hilo kwani linamvunjia heshima mchumba wake Chioma pamoja na familia yake kwani ni watu wenye malengo ya kuingia kwenye ndoa hivi karibuni.

Kupitia Instastory  yake Davido ameweka maelezo yaliyosomeka…>>> “Nyie wote mnafahamu kuwa nimeshamchumbia mpenzi wangu Chioma, haitakuwa na maana kwa mimi kufanya hivyo mnavyosema, Mama wa mtoto wangu alikuwa na bishara ya bidhaa za nywele Ghana, na mimi hivyo hivyo nilikuwa nimealikwa kuburudisha kwenye Afronation, hivyo nikampa lifti mpaka Ghana”

“Sijaelewa kwanini mnasambaza taarifa za uongo, mnajua hazitafanya kitu ila zimeniumiza na kuishushia heshima familia yake, 2020 ni kwaajili ya mambo chanya tu” – Davido

WASTARA NA MIAKA SABA YA KIFO CHA SAJUKI , AKUMBUKA HAYA

Soma na hizi

Tupia Comments