Habari za Mastaa

Tarehe ya ujio wa album mpya ya Davido imenifikia mtu wangu!

on

Boss wa lebo ya HKN Music Davido kutoka Nigeria anazidi kuionyesha dunia uwezo wake, baada ya kushindwa kutoa album yake mpya September mwaka hu, mwenyekiti wa lebo hiyo ambaye pia ni kaka wa msanii huyo Adewale Adeleke ametangaza tarehe ya uzinduzi wa Album mpya ya Davido ‘Baddest’.

daavido3

Kama wewe ni shabiki mkubwa wa muziki wa Davido basi hii good news ikufikie mtu wangu… Album mpya ya Davido ‘Baddest’ itakuwa sokoni tarehe 10 mwezi huu yani siku tano kuanzia leo!

daavido4

Hapo awali Album hiyo iltangazwa kutoka tarehe 8 June lakini badaade ikasogezwa mbele mpaka tarehe 8 August lakini pia ikashindikana na kupangwa kutoka September japo tarehe haikutajwa… ila sasa taarifa zilizo rasmi ni kwamba album ya ‘Baddest‘ itakuwa mtaani tarehe 10 October.

daavido2

Kizuri zaidi ni kwamba kwenye Album hii mpya Davido kafanya kazi na mastaa wakubwa wa muziki Marekani baadhi ni kama Meek Mill, Trey Songz na Akon!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,TWITTER,FB, YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments