Habari za Mastaa

Kuelekea countdown ya birthday yake, Davido ameamua kujizawadia ndinga hii mpya! (+Pichaz)

on

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Davido anazidi kuonyesha uwezo wake wa kuchop money kadri siku zinavyoenda… zimebaki wiki kama mbili kufikia tarehe 21 Novembeer 2015, siku ya kuzaliwa kwa Mkurugenzi wa HKN Music, David Adeleke.

Tarehe 21 November 2015, Davido atakuwa anatimiza miaka 23, na staa huyo wa muziki kutoka Nigeria ameamua kujizawadia mapema ikiwa ni sehemu ndogo ya maandalizi kuelekea siku yake kubwa.

R82

Mkurugenzi huyo wa HKN Music kaamua kujizawadia toleo jipya la gari, Audi R8 ambalo kwa mujibu wa jarida la Car Magazine, Audi R8 ni miongoni ya magari ya kisasa zaidi yani ‘2015 supercar’ kwa mwaka 2015… kupitia page yake ya Instagram, Davido alipost picha ya gari hilo na caption iiyosema…

>>> “ Early birthday gift to myself!! My R8!! Finally here!!!!! THANK GOD for his continuous BLESSINGS!! Watch wat comes next!!! @benzaiautogroup THANK YOU! ” <<< @davidoofficial.

R8

Gari jipya la Davido, Audi R8 linaongeza namba ya idadi ya magari aliyonayo msanii huyo, inawezekana unajua ama hujui ila staa huyo wa muziki kutoka Nigeria ana jumla ya magari saba ya kifahari kufikia mwaka 2015, ukitoa hili jipya mengine aliyonayo Davido ni pamoja na…

1. Mercedes G-Wagon.

DAVIDO8
2. 2015 Range Rover Sport SUV.

DAVIDO11
3. 2012 Audi Q7.

DAVIDO4
4. Chevrolet Camaro.

DAVIDO6
5. 2012 Honda

DAVIDO9
6. Porsche Turbo.

DAVIDO10

Gari jeupe kwenye hii picha ndio Porsche Turbo miongoni mwa yale saba ya kifahari ya Davido.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments