Msanii wa Filamu Halima Mpinge (Davina) Chini ya Taasisi yake ya SHADA ORGANIZATION Kwa kushirikiana na Chama Cha Waigizaji Mkoa wa Iringa wameazimisha siku maalumu ya Wapenda nao Kwa kukabidhi Vifaa vya kujifungulia Kwa Wakina Mama Wajawazito katika Kituo Cha Afya Ihongole kilichopo Halmashauri ya Mji Mafinga ikiwa ni sehemu ya kuonesha upendo Kwa Jamii.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Davina amesema Lengo kubwa la kufanya hivyo ni kuonesha upendo Kwa Jamii hasa Kwa wenye Uhitaji huku akisema kuwa jumla ya msaada huo umegharimu Shilingi milioni nne.
Naye Msimamizi wa Kituo hicho Cha Ihongole Peter Mwachula amesema Vifaa hivyo vitakwenda kuwa Mkombozi Kwa Wakina Mama Wajawazito kwani awali Kulikuwa na uhaba wa Vifaa hivyo huku akiwaomba Wadau wengine kuweza kujitokeza kwa wingi ili kusaidia Juhudi za Serikali katika kuboresha utoaji huduma za afya.
Akizungumza Kwa niaba ya Wasanii Mwenyekiti wa Chama hicho Cha Waigizaji Khamis Nurdin amewataka Wadau mbalimbali kujenga utamaduni wa kuwakumbuka wenye Uhitaji.