Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama amesema tayari dawa ambayo imetengenezwa na vijana aliowaibua wilayani humo na kuipa jina la Baycaro Kiboko ya Corona, imethibitishwa na NIMR kuwa ina uwezo wa kupambana na virusi mbalimbali ikiwemo vya corona lakini pia kansa na uvimbe, Mshama amesema dawa hiyo inakinga na kutibu pia.
“Dawa ya corona (Baycaro) tuliyowaambia tunaipeleka kuifanyia vipimo kule NIMR, cha kumshukuru Mungu vipimo vimerudi na imeonekana inafaa kwahiyo inatuhalalishia kwamba Watu hawatokufa tena, tunaweza kuwa sawa na Madagascar, kitendo cha kutibu saratani, virusi na uvimbe katika mwili maana yake ni dawa kubwa sana, haiwezi kuua Mtu” -DC MSHAMA
“Ukinywa haujapona unasema tu kama ni hela yako unarudishiwa, ndio maana unaniona sijavaa barakoa, wewe ambaye haujanywa dawa yoyote vaa barakoa, kama Madagascar wamepata dawa Why not Tanzania?, kwakuwa haina sumu tutaanzia hapa kwetu tutaongea na RMO aruhusu Watu (wagonjwa corona) wanywe”- DC MSHAMA