Polisi wamepata kiasi kikubwa cha fentanyl, madawa ya kulevya na vifaa vingine vilivyofichwa chini ya mlango wa shule ya chekechea ya New York City baada ya siku chache kupatikana kwa kifo cha mvulana kutokana na kuathiriwa na dawa ya kulevya aina ya opioidi.
Picha zilizotolewa na Idara ya Polisi ya Jiji la New York zinaonyesha zaidi ya mifuko kumi na mbili ya plastiki iliyojaa ungaunga wa rangi ya kahawia na nyeupe.
Uchunguzi unaendelea, polisi walisema.
Mtoto wa mwaka mmoja alifariki kwa kushukiwa kuwa ametumia dawa za kulevya kupita kiasi katika kituo cha kuangalia watoto siku ya Ijumaa iliyopita.
Nicholas Dominici alikuwa katika kitalu cha Divino Niño kwa wiki moja tu. Fentanyl alikuwa amefichwa kwenye chumba cha kulala chini ya mkeka alipokuwa akilala, polisi walisema.
Nicholas Dominici alikuwa katika shule ya chekechea ya Divino Niño kwa wiki moja tu. Dawa ya kulevya ya Fentanyl ilikuwa imefichwa kwenye chumba cha kulala chini ya mkeka alipokuwa akilala, polisi walisema.
Watoto wengine watatu walilazwa hospitalini baada ya kuathiriwa na dawa hiyo ya kulevya katika kituo hicho.
Uchunguzi wa mkojo kutoka kwa mmoja wa waathiriwa ulithibitisha uwepo wa dawa hiyo.
Mmiliki wa shule hiyo, Grei Mendez, 36, na mpangaji wake, Carlisto Acevedo Brito, 41, wanakabiliwa na mashtaka ya serikali ya kumiliki dawa za kulevya kwa nia ya kusambaza na kusababisha kifo, na mashtaka ya kula njama, kulingana na waendesha mashtaka.